CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya.

CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Jacob John Mkunda, amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa maono ya kuanzisha Kampuni ya Bima ya Maisha (SUMAJKT Life Insurance Co. Ltd) itakayokuwa Msaada mkubwa kwa Watanzania kwa Vizazi vya sasa na Vijavyo.

Jenerali Mkunda, ameyasema hayo Tarehe 10 Mei 2025 katika Sherehe ya Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Maisha ya SUMAJKT tukio lililofanyika Ukunbi wa (The Super Dome Masaki Jijini Dar es salaam. CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya.

Amesema imani yake ni kuona watanzania wakipatiwa huduma hiyo ya Bima kwani Jeshi la Kujenga taifa kupitia Shirika lake SUMAJKT limekua likitoa huduma stahiki kwa wateja kupitia, Kampuni zake tanzu, Viwanda, pamoja na Miradi ya kibiashara.

Aidha Jenerali Mkunda ametoa wito kwa watanzania kuitumia kampuni ya Bima ili waweze kupata suluhisho la changamoto zao za kibima. CDF aipongeza SUMAJKT kwa kuanzisha kampuni mpya.

Naye Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, amesema Kampuni ya Bima ya SUMAJKT tayari imesajiliwa, huku akiahidi utolewaji wa huduma bora za viwango stahiki.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya SUMAJKT, Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu), Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi na Makao Makuu ya JKT, Wakuu wa Vyuo na Shule, Maafisa Jenerali, Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, Mwenyekiti wa Umoja wa Kampuni za Bima Tanzania (ATI) Bi. Flora Minja, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Bima ya SUMAJKT Meja Godson Mhando, Maafisa wakuu, Maafisa Wadogo, Askari, Wageni waalikwa na Waandishi wa Habari.

Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *