|

Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu

Maafisa UPDF watembelea SUMAJKT Makao Makuu. Maafisa Jenerali, Maafisa wakuu na Askari kutoka Jeshi la Uganda (UPDF) wakiongozwa na Meja Jenerali Willium Nabasa, leo tarehe 29 Aprili 2025 wametembelea Makao Makuu ya SUMAJKT Mlalakuwa Dar es Salaam ili kujifunza shughuli za Jeshi la Kujenga Taifa na SUMAJKT kwa manufaa ya kuliendeleza Jeshi la Uganda.

Maafisa hao wamepokelewa na Mkuu wa Shule ya Jitegemee Kanali Emmanuel Mwaigobeko, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele.

Akizungumzia ugeni huo Kanali Mwaigobeko, amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza Shughuli zinazofanywa na JKT pamoja na SUMAJKT.

Jeshi la Kujenga Taifa kupitia Shirika la Uzalishaji Mali SUMAJKT hupokea ugeni kutoka nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kujionea na kujifunza shughuli za kiuchumi zinazofanywa na Shirika hilo.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *