Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT. Mkuu wa Tawi la Mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Kanali Longinus Nyingo tarehe 16 Aprili 2025 amekagua Maandalizi ya Mwisho kuelekea kuhitimishwa kwa zoezi la Ufungaji wa Mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa Kujitolea Operesheni Miaka 60 ya Muungano katika Kikosi cha Ruvu JKT Mlandizi mkoani Pwani.
Kanali Nyingo amesema kuwa, zoezi la ufungaji wa Mafunzo katika Vikosi vyote vya JKT lilianza tarehe 8 Aprili 2025 ambapo Mkuu wa JKT alikuwa akiwakilishwa na Wakuu wa Matawi na Wakurugenzi kutoka Makao Makuu ya JKT, kesho tarehe 17 Aprili 2025 zoezi hilo litahitimishwa na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kikosi hapo. Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele kuhitimisha Ufungaji wa Mafunzo ya Vijana wa Kujitolea OP Miaka 60 ya Muungano Ruvu JKT.
Nae Kamanda Kikosi Ruvu JKT Kanali Peter Mnyani Amewakaribisha wananchi wa Mkoa wa Pwani na Maeneo jirani kwenda kushuhudia Vijana wao wakihitimisha Mafunzo yao.
Katika kukuza utalii wa ndani, Kanali Mnyani ametumia wasaa huo kuwakaribisha wananchi kutembelea bustani ya Wanyama pori walio wapole ya RUVUJKT WILDLIFE.
Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube
https://www.instagram.com/p/DIHNoSIIeOh/?igsh=MWlvM29jeGUwMWNvMQ==
chanzo: https://www.instagram.com/reel/DIgxcR1oD_b/?igsh=OGtjcHVnN2V4Nm1z