Ugeni wa Wakufunzi na Wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa nchini Nigeria (NDC) Wafanya ziara ya Kimasomo Katika Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT)
Ugeni wa Wakufunzi na Wanafunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa nchini Nigeria (NDC) Wafanya ziara ya Kimasomo Katika Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Mlalakuwa Dar es salaam, leo tarehe 04 Machi 2025 kwa lengo la kujifunza namna Shirika linavyofanya Shughuli za Uzalishaji wa Bidhaa hususani Viwandani.
Ugeni huo wa Wakufunzi na wanafunzi idadi 26 ukiongozwa na Mkuu wa Msafara ‘ Air Vice Marshal’ Hanidu Ibrahim, umepokelewa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele.





Akizungumza baada ya Ziara hiyo, ‘Air Vice Marshal’ Ibrahim amebainisha wamehamasika na uzalishaji unaofanywa na SUMAJKT kupitia kiwanda cha Taa, Maji, Ushonaji Nguo na Bidhaa za Ngozi.
“Lengo la ziara yetu ni Kujifunza Shughuli zinazofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa na Shirika lake SUMAJKT na namna linavyochangia katika Uchumi wa Tanzania, hivyo tumejifunza Mengi tutaenda kuyatumia katika Kujenga Uchumi wa Taifa letu Nigeria” amesema.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Kanali Shija Lupi amesema Ugeni huo umeridhishwa na kazi za SUMAJKT.
Ugeni huo umepata fursa ya kutembelea Kiwanda cha Taa (SUMAJKT Skyzon Co.Ltd), Kiwanda cha Maji (SUMAJKT Bottling Co.Ltd), Kiwanda cha Ushonaji Nguo (SUMAJKT Garments Co.Ltd) na Bidhaa za Ngozi.