|

Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi

Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Daniel Sillo ayashauri mashirika ya Kijeshi ndani ya Nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Sayansi na Teknolojia katika uzalizalishaji wa bidhaa zao.

Mhe. Sillo amesema hayo leo tarehe 25 Februari 2025 alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Mashirika yanayo milikiwa na  Majeshi ya  nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Geraffe iliyopo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Mambo ya Ndani ayashauri mashirika ya Kijeshi, Amefafanua kuwa Mkutano huo hufanyika kila mwaka ili kutathmini utendaji kazi wa Mashirika na Viwanda vilivyopo ndani ya Majeshi yaliyopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilizoshiriki mkutano huo ni nchi mwenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Demokrasia Congo, Sudan Kusini na Somalia.

Pamoja na kikao hicho wajumbe wa kikao kesho watatembelea Kiwanda cha Taa cha SUMAJKT Skyzon Co. Limited na maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na mashirika ya Jeshi nchini Tanzania katika viwanja vya Golf Club Dar es Salaam.

Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *