DKT. STERGOMENA TAX AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI ENEO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA KIKOMBO DODOMA
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 31 Januari 2025, amewaongoza Maafisa, Askari, Vijana na Watumishi wa Umma katika zoezi la upandaji miti katika eneo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo pamoja na eneo la viwanja vya makazi ya watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Chinangali 2 nje kidogo ya Jiji la Dodoma.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upandaji miti, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema zoezi hilo ni muendelezo wa kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan za upandaji miti mwezi Januari ya kila mwaka.
Zoezi hilo la Upandaji miti ya matunda na kivuli Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo, limehudhuriwa pia na Mkuu wa Tawi la Lojistiki na Uhandisi Jeshini, Meja Jenerali Hawa Kodi na baadhi ya Maafisa na Askari kutoka Makao Makuu ya Jeshi pamoja na Makamishna toka Makao Makuu ya Wizara, Wakuu wa Idara na Vitengo, Vijana wa JKT pamoja na Watumishi wa Umma.
https://www.instagram.com/p/DFf7NcHIsp2/?igsh=MXhlcTBxeGd5ZnQ1Mg==