SUMAJKT LAJIWEKEA MALENGO MWAKA WA FEDHA 2024/’25

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) limeweka malengo ya kufikika na linaendelea kusimamia miradi kwa ufanisi ili kuleta tija kwa shirika.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya (SUMAJKT) Meja Jenerali (mstaafu) Farah Mohamed, amesema hayo tarehe 19 Oktoba 2024 katika kikao cha kwanza cha malengo ya shirika cha mwaka wa fedha ujao wa 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa SUMAJKT Tower uliopo jijini Dodoma.

Kikao hicho kilihudhuriwa wajumbe wa Bodi akiwemo Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata pamoja na wajumbe waalikwa kutoka JKT na SUMAJKT.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *