huduma na biashara

  • SUMAJKT, NYUMBU NA MZINGA KUENDELEZA USHIRIKIANO

    Kamishna wa Maendeleo na Utafiti Wizara ya Ulinzi na JKT Rear Admiral Michael Mumanga, amewataka wakuu wa Mashirika ya Kijeshi ya TATC -Nyumbu, Mzinga na SUMAJKT kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuibua fursa zitakazo ongeza maendeleo zaidi katika mashirika hayo. Rear Admiral Mumanga, amesema hayo Oktoba 23, 2025 katika kikao cha wakuu wa Mashirika ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kilichofanyika Makao Makuu ya SUMAJKT Dar es Salaam. Aidha, Rear Admiral Mumanga, amefafanua lengo la kikao hicho ni kushirikiana kwa mashirika pamoja Wizara ya Ulinzi na JKT ili kuongeza mafaninikio ya mashirika hayo ambayo ni SUMAJKT, Nyumbu na Mzinga….

  • DED SUMAJKT atembelea Mafinga.

    DED SUMAJKT atembelea Mafinga. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Shija Sahani Lupi ametembelea Miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika Halimashauri ya mji mdogo Mafinga Mkoani Iringa. Tukio hilo limejiri tarehe 17 Oktoba 2025 mara baada ya kushiriki Mahafali ya 29 ya kidato cha Nne katika shule ya Sekondari Kawawa JKT akiwa Mgeni rasmi. Brigedia Jenerali Lupi ametembelea Majengo ya madarasa mapya yatakayotumika kujifunza kwa njia ya mtandao (E-learning), shule ya Awali na Msingi, eneo la shamba jipya la mifugo (Ng’ombe) na baada ya kutembelea maeneo hayo alipata fursa ya kuongea…

  • Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT

    Meja Jenerali Mabele Ampokea mkuu wa JKT Zambia makao makuu SUMAJKT. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amepokea ugeni wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kutoka nchini Zambia Luteni Jenerali Maliti Solochi, ambaye amefanya ziara Makao Makuu ya SUMAJKT ili kubadilishana uzoefu katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo. Ugeni huo baaba ya kupokelewa leo tarehe 28 Aprili 2025 umetembelea Kiwanda cha SUMAJKT Skyzon Co. Ltd, Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi na Mradi wa SUMAJKT Energies ili kujionea shughuli za…

  • Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu), aongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri ya SUMAJKT

    Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu), aongoza Kikao cha Bodi ya Ushauri ya SUMAJKT kupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika leo tarehe 14 Machi 2025 katika ukumbi wa Mebele jijini Dodoma. Lengo la kikao hicho ni mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kupitisha makadirio ya bajeti ijayo ya mwaka wa fedha wa 2025/2026. Kikao hicho cha Bodi ya Ushauri SUMAJKT kimehudhuriwa na Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Meja Jenerali Rajabu Mabele,…

  • Kampuni ya usafi SUMAJKT yasaini mkataba na Halmashauri ya Jiji Dar

    Kampuni ya Usafi na Unyunyiziaji Dawa ya SUMAJKT Cleaning and Fumigation Co. Ltd  imetia Saini Mkataba wa kufanya Usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Katika Maeneo ya Soko la Buguruni Pamoja na Soko la Ilala leo tarehe18 Februari 2025. Hafla hiyo ambayo  imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mhe. Elihuruma Mabelya, Mstahiki Meya wa Jiji Mhe. Omary Kumbilamoto, Madiwani, na wadau wa Maendeleo imehusisha pia Uzinduzi wa Magari yaliyo nunuliwa na jiji yatakayotumika Katika Usafi. Akizungumza mara baada ya Kutia Saini Mkataba huo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Jonas Mpogolo,…