SUMAJKT Leather Products
Kiwanda cha bidhaa za ngozi SUMAJKT Leather Products kipo eneo la Mlalakuwa, jijini Dar es Salaam na kinajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa za ngozi kwa ajili ya matumizi ya taasisi za ulinzi, shule, kampuni, pamoja na watu binafsi. Bidhaa zinazozalishwa ni pamoja na viatu, mikanda, mabegi na mikoba.
Kiwanda hiki kilianzishwa rasmi tarehe 13 Julai 2017. Aidha, Kiwanda kilianza kwa kutumia moja ya majengo yaliyokuwa Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa Mlalakuwa Dar es Salaam na vyerehani vilivyokuwa vinatumiwa na Kampuni ya CAMISUMA kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa za ngozi.
Kwa sasa kiwanda kimefanikiwa kununua vyerehani na mashine za kisasa za kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali.
Fanya kazi nasi leo
Tembelea ofisi zetu au bofya kitufe hiki kupata mawasiliano yetu..