SUMAJKT Garments Co LTD
Hii ni kampuni ya Shirika inayojishughulisha na ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali kwa ajili ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama, makampuni na watu binafsi kilichopo Mgulani JKT jijini Dar es Salaam.
Kiwanda kilianza uzalishaji rasmi tarehe 22 Aprili 2017 na kusajiliwa kuwa Kampuni ya Ushonaji SUMAJKT Garments Co. Ltd mnamo 27 Februari 2020. Kiwanda kimenunua mashine mpya na kuendelea kutumia majengo na baadhi ya mashine zilizoachwa na Kiwanda cha CAMISUMA kilichofungwa mwaka 2010.
Kampuni imekua mstari wa mbele katika kupunguza gharama za upatikanaji wa mavazi ya kijeshi kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la kujenga Taifa(JKT), Jeshi la Akiba (JA) na Jeshi la Uhifadhi (TFS, TANAPA, TAWA na NCAA). Taasisi mbalimbali, mashirika na watu binafsi wanapata huduma ya ushonaji mavazi katika kiwanda cha SUMAJKT Garments Co. Ltd.
Kampuni ya Ushonaji ya SUMAJKT Garments Co. Ltd zilizinduliwa rasmi tarehe 17 Mei 2018 na Hayati Dkt. John Joseph pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu. Aidha, wakati wa uzinduzi huo ilitangazwa eneo la Mgulani JKT kuwa Kituo cha Uwekezaji cha JWTZ.
Fanya kazi nasi leo
Tembelea ofisi zetu au bofya kitufe hiki kupata mawasiliano yetu..