Mradi wa SUMAJKT Agri-Machinery
Mradi huu ni matokeo ya juhudi za Serikali zilizofanywa katika kutekeleza mpango wa kuinua sekta ya kilimo kupitia kauli mbiu ya “Kilimo Kwanza” mwaka 2009 kutokana na juhudi za Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
Shirika katika mpango huo lilipewa jukumu la kupokea kutoka Serikalini na kusambaza matrekta na zana za kilimo zilizonunuliwa kutoka nje.
Hivyo, JKT kupitia Shirika lilianzisha mradi wa matrekta ili kutekeleza jukumu hilo la Serikali.
Mradi huu umekuwa msaada kwa wakulima tangu kuanzishwa kwake kwani wengi wamefaidika kupitia huduma ya Matrekta na zana zake.
Aidha, huduma ya kusambaza matrekta, zana na vipuri vyake umesaidia kuanzisha mradi wezeshi wa kuuza matrekta, vipuri na zana za kilimo kwa njia ya fedha taslimu.
Mradi huu umewawezesha wakulima nchini kufaidika kwa kupata uelewa wa matumizi juu ya zana za kilimo, kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na ajira hasa maeneo ya vijijini.
Pia, mradi unatekelezwa kwa kukusanya madeni kwa watu na taasisi zilizopewa Matrekta na vipuri.
Matrekta na zana hizo ni; Matrekta ya New Holland na FARMTRAC, majembe ya kulimia (Disc Plough), jembe la kuvunja udongo (Disc harrow), pump za umwagiliaji (Irrigation water pump) na tela (Trailer).
Dhima Yetu
Kuimarisha maendeleo ya kilimo na kukuza tija kupitia matumizi sahihi ya mashine za kilimo ili kuhakikisha upatikanaji wa mazao ya biashara na chakula kwa taifa na kuboresha maisha ya kilimo.
Malengo yetu
- Kuongeza matumizi ya matrekta na zana nyingine zinazofanana na hizo katika kilimo.
- Kuzalisha na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo.
- Kuhakikisha usalama wa chakula kwa watu na taifa zima kwa ujumla.
- Kuongeza fursa za ajira kwa wananchi wa mijini na vijijini.
Fanya kazi nasi leo
Kwa huduma bora za matrekta na zana za kilimo, wasiliana nasi kupitia:
Sanduku La Posta 1694,
Dar Es Salaam, Tanzania.
Simu/WhatsApp/Hotline: +255 786 610 881
Email: agrimachinery@sumajkt.go.tz
au fika katika ofisi zetu zilizopo New Bagamoyo Road, Mwenge light Indutries jijini Dar es salaam, Tanzania.