Meja Jen. Mabele aikaribisha SUA Makao Makuu ya JKT Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, ameukaribisha Makao Makuu ya JKT Uongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ili kufanya mazungumzo ya namna ya kuboresha Sekta ya Kilimo ndani Jeshi la Kujenga Taifa.

Meja Jenerali Mabele ametoa ukaribisho huo leo tarehe 31 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, baada ya kufanyika kikao cha Utekelezaji wa Makubaliano kati ya JKT na SUA juu ya Mpango wa Mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Chuo hicho.

Nae Dkt. Nyambelila Amouri kutoka RASI NDAKI ya Kilimo SUA mkoani Morogoro amesema, kupitia kikao hicho na ushirikiano uliopo kati ya JKT na chuo cha SUA, kikao kimeonyesha mafanikio makubwa na kinachofuata ni utekelezaji wa Makubaliano hayo.

Aidha, amesema kupitia kikao hicho pia, wanafunzi wa SUA wataongeza wigo wa maeneo ya kufanya mafunzo kwa vitendo ndani ya JKT.

https://www.instagram.com/p/DFf5O2XIMXo/?igsh=MXg3NHAyenV6M2ph

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *