Tunu Zetu

Utaalamu (Professionalism)

Tunazingatia viwango vya juu vya umahiri, nidhamu, na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yetu yote.

Utendaji (Performance)

Tunajikita katika kufikia matokeo bora kwa kutumia rasilimali kwa ufanisi na kutimiza malengo yaliyowekwa.

Uadilifu (Integrity)

Tunatenda kwa uaminifu, maadili mema, na uwazi katika maamuzi na vitendo vyetu, huku tukiwajibika kikamilifu kwa matokeo.

Ubunifu (Innovation)

Tunahamasisha mawazo mapya na maboresho endelevu ili kuongeza ubora wa huduma na tija ya shirika.

Uwajibikaji kwa wateja (Responsiveness)

Tunatoa huduma kwa wakati, kwa ubora unaotakiwa, na kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na jamii.