Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa

Mkurugenzi SUMAJKT awataka Watendaji kutumia fursa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) Brigedia Jenerali Petro Ngata amewataka Wakurugenzi Waendeshaji, Wakuu wa Shule na Miradi kutumia vizuri fursa zilizopo katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija kwa Shirika.

Brigedia Jenerali Ngata ameyasema hayo tarehe 15 Agosti 2025 katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya SUMAJKT (KUS) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Brigedia Jenerali Ngata amehimiza kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo ya Shirika.

Aidha, amewasisitiza kuendelea kuzalisha Bidhaa na kutoa huduma katika ubora ili kuendelea kuilinda imani ya wananchi waliyonayo kwa SUMAJKT.

Vilevile amewakumbusha kuendelea kutekeleza Majukumu yao kwa Weledi na Uaminifu.

Brigedia Jenerali Ngata amehitimisha Kikao hicho kwa kuwapongeza Wakurugenzi Waendeshaji wa Kampuni Tanzu za SUMAJKT, na Wakuu wa Shule wanaofanya vizuri na kuwataka kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha zaidi ili Shirika lizidi kusonga mbele.

Kamati ya Utendaji SUMAJKT hufanya Kikao kila mwezi kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa shughuli za Uzalishaji Mali zinazofanywa na Shirika hilo.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *