DC IKUNGI AVUTIWA NA MAONESHO YA JKT NANE NANE
DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe.Thomas Cornel amevutiwa na Bidhaa na Huduma za Jeshi la Kujenga Taifa katika maonesho ya Wakulima Nanenane yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nzuguni Dodoma.
Akizungumza baada ya kutembelea Banda la JKT leo tarehe 6 Agost 2025, Mhe. Cornel amepongeza JKT kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali yanayosaidia upatikanaji wa chakula cha asili kinachokidhi viwango vya soko la kimataifa. DC Ikungi avutiwa na maonesho ya JKT Nane Nane.
Vilevile, Mhe. Cornel amepongeza JKT na Shirika lake SUMAJKT kwa Ubunifu wa bidhaa mbalimbali na Utekelezaji mzuri wa Miradi ya Ujenzi.
Aidha, Mhe Cornel amefurahishwa na Vijana wa JKT namna wanavyoshiriki katika Uzalishaji Mali, hivyo ametoa wito kwa wazazi kuruhusu vijana wao kujiunga na Jeshi hilo ili kupata ujuzi katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.







Mhe. Thomas Cornel alipokelewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nanenane Kitaifa wa JKT Kanali Shija Lupi na kumpitisha katika Banda la JKT, ambapo amejionea Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Vikosi, Chuo, Shule na Kampuni Tanzu za SUMAJKT.