Wanafunzi kutoka Nigeria wafurahishwa na shughuli za SUMAJKT

Wanafunzi kutoka Nigeria wafurahishwa na shughuli za SUMAJKT. Ugeni wa Wakufunzi na wanafunzi chuo Cha Taifa Cha Mafunzo ya Usalama nchini Nigeria wafurahishwa na Shughuli za Jeshi la Kunega pamoja na Shirika lake SUMAJKT. Ugeni huo wa Wakufunzi na wanafunzi idadi 25 ukiongozwa na Mkuu wa Msafara huo Makamu Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mafunzo Bwana Hyginus Ngele Umepokelewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa jijini Dar es salaam tarehe 18 Juni 2025.

Akizungumza Mkuu wa Msafara Bwana Hyginus Ngele baada ya Kupata taarifa fupi ya Shughuli za JKT na kutembelea kiwanda maji ameeleza namna alivyofurahishwa na Shughuli hizo za Uzalishaji.

“Kiwamda cha Maji cha SUMAJKT B Co. Ltd ni jitihada kubwa za Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa kutumia nguvu kazi na mitaji katika kuwekeza, kiukweli tumejionea namna uzalishaji unavyofanyika inapendeza.

Pia utaratibu wa kuchukua vijana, kuwalea na kuwajengea uzalendo ni mzuri kwa Ujenzi wa Taifa.

Ni jambo zuri kuona Hata Mavazi ya Jeshi la Ulinzi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania yanashonwa na kiwanda cha SUMAJKT kwani hata Watendaji wanavaa mavazi wanayozalishaji wenyewe katika viwamda vyao kwakweli jambo hili linapaswa kuigwa hata kwa nchi yetu Nigeria, Tutaenda kushauri”

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Kanali Shija Lupi ameleeza kuhusu ziara hiyo.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *