JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu waliobainika na watakaobainika kughushi vyeti

Jeshi la Kujenga Taifa JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu waliobainika na watakaobainika kughushi vyeti vya kuhitimu mafunzo. JKT imefikia uamuzi huo baada ya kubaini uwepo wa vyeti vya kughushi vilivyotumiwa na baadhi ya vijana ambao siyo waaminifu ili kujipatia ajira katika taasisi na
kampuni zinazohitaji watendaji waliopitia mafunzo ya jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala, Kanali Juma Mrai amesema Jeshi la Kujenga Taifa lipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi na kampuni zote zinazohitaji uhakiki wa vyeti kwa watumishi wao waliopitia mafunzo ya JKT. JKT limesema litawachukulia hatua za kisheria watu waliobainika na watakaobainika kughushi vyeti.

Jeshi la Kujenga Taifa pia limesisitiza kuwa nafasi za kujiunga na mafunzo ya JKT zinatolewa kila mwaka kwa vijana wa kitanzania wenye sifa, ili wakimaliza mafunzo hayo wapate cheti.

Pia, limewakumbusha wananchi kuwa nafasi hizo zinatolewa kwa kutangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii nchini, hivyo waepuke kutapeliwa kwa kutumiwa ujumbe mfupi katika simu zao, kupigiwa simu na kutakiwa kutoa kiasi fulani cha fedha ili kupata nafasi hizo.

Endelea kutufuatilia kupitia website yetu ya https://sumajkt.go.tz/ na mitandao yetu ya kijamii ya facebook, Instagram na Youtube

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *