MKUU WA JKT AISHUKURU SERIKALI KULIWEZESHA JKT KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa kutekeleza majukumu yake
Meja Jenerali Mabele ametoa shukrani hizo tarehe 16 Januari 2025 Makao Makuu ya JKT wakati wa hafla ya uzinduzi wa Magari aina ya Isuzu D Max Pick Up idadi tisa (9) kwaajili ya Matumizi ya shughuli za kiutawala ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Magari hayo yamekabidhiwa kwa baadhi ya Wakurugenzi wa Makao Makuu ya JKT na Makamanda Vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa.