Waziri wa Ulinzi Angola, aridhishwa na shughuli za SUMAJKT

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Angola Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameridhishwa na shughuli zinazofanywa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga (SUMAJKT).

Akizungumza baada ya kufanya ziara SUMAJKT leo tarehe 11 Januari 2025, Mhe. Dos Santos, amebainisha kuwa amevutiwa na uzalishaji unaofanywa na Shirika hilo, hivyo wataenda kufanyiakazi nchini kwao.

“Wizara yetu ya Ulinzi nchini Angola kupitia Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania tutakuja kusaini hati ya awali ya makubaliano ambayo itaonesha maeneo ya kushirikiana” alisema Mhe. Dos Santos.

Aidha, Mhe. Joao Ernesto Dos Santos, ameishukuru Wizara ya Ulinzi na JKT Tanzania kupitia JWTZ kwa kuwezesha ziara hiyo ambayo imekuwa na manufaa kwao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa JKT na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, amesema Mhe. Joao Dos Santos, ameridhishwa na Teknolojia inayotumika katika uzalishaji wa bidhaa ikiwemo kiwanda cha Taa (SUMAJKT Skyzon Company Ltd), Kiwanda cha Maji ya Kunywa ya Uhuru Peak (SUMAJKT Bottling Co.Ltd) na Kiwanda cha Ushonaji nguo (SUMAJKT Garments Co. Ltd).

SUMAJKT imekuwa ikitembelewa na ugeni kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kuona na kujifunza uzalishaji unaofanywa na Shirika hilo.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *