Waziri wa Ulinzi Comoro atembelea SUMAJKT Makao Makuu

Waziri wa Ulinzi ambaye pia ni Katibu wa Rais nchini Comoro Mhe. Yousoufa Mohamed Ali ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) ikiwa ni Mwendelezo wa Mazungumzo ya kushirikiana katika biashara baina ya Shirika Hilo na Comoro.

Mhe. Yousoufa akiwa ameongozana na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania – Comoro Khalfan Saleh amepokelewa na Kanali Robert Kessy kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata Makao Makuu Mlalakuwa Jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe, ziara hiyo ya Mhe. Yousoufa Mohamed Ali imetokana na Makubaliano ya Awali ya kibiashara kati ya SUMAJKT na Visiwa vya Comoro ambapo Tarehe 07 Oktoba 2024 Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja Mhe. Mze Mohamed Ibrahim alisaini hati ya Makubaliano ya kushirikiana kibiashara Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Dar es salaam.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *