Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aongoza waombolezaji kumuaga Meja Jenerali Charles Mbuge

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 16 Octoba, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam ameongoza Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na waomboleazaji, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge, aliyefariki Dunia tarehe 12 Octoba 2024.

Miongoni mwa viongozi walioungana na Waziri wa Ulinzi na JKT kumuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenerali Mbuge, ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Albert Chalamila, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi La Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Salum Othman, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Venance Mabeyo, na viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na Taasisi nyingine za Serikali na Kiraia.

Mwili wa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Charles Mbuge umesafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa mazishi tarehe 17 Octoba, 2024.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *