|

Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja atembelea SUMAJKT

Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja nchini Comoro Mhe. Mze Mohamed Ibrahim atembelea SUMAJKT akiangalia Bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT.

Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata akimpokea Gavana wa Ngazidja, Mze Mohamed Ibrahim alipowasili Makao Makuu ya SUMAJKT.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata alimpokea Gavana wa Ngazidja Mze Mohamed Ibrahim baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), tarehe 05 Octoba 2024. Ambapo Ugeni huo Ulikuja Tanzania kwa ajili ya Mahusiano ya kibiashara na SUMAJKT.

Akiambatana na ujumbe kutoka Comoro, Gavana alipata wasaa wa kutembelea na kujionea bidhaa mbalimbali katika Banda la Maonesho ya Bidhaa na Huduma alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Mlalakuwa Dar es salaam.

Taarifa zaidi kuhusu ugeni huo imewekwa katika chaneli ya YouTube ya SUMAJKT hapa chini;

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *