SUMAJKT Insurance Broker Co. Ltd

Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2019 ili kutoa huduma ya bima za magari, afya, ajali, nyumba, safari za majini, biashara na maisha.


Makao Makuu yake yapo Mgulani, jijini Dar es Salaam.

Lengo la kuanzishwa kwake ni kusaidia Shirika katika kuongeza mapato kwa kutumia fursa ya wateja waliopo ndani na nje ya Jeshi.

sumajkt auction mart
SUMAJKT Logistics

Kuanzishwa kwake kulitokana na hitaji la makampuni na miradi mbalimbali ndani ya Shirika ikiwemo miradi ya ujenzi, ulinzi
pamoja na huduma ambazo husababisha Shirika kutoa fedha kwa makampuni mengine ya huduma za bima.

Kampuni inajikita kutanua soko kwa kutafuta kazi za nje ya Jeshi hasa kwenye taasisi, makampuni, na watu binafsi ambapo kazi zinatekelezwa kwa gharama iliyopangwa na Kamishna wa Usimamizi wa Bima Nchini kwa ufanisi mkubwa.

DIRA YEU

Kuwa kampuni inayoheshimika na inayoongoza nchini katika kutoa huduma zote za uwakala wa bima.

Dhima Yetu

Kuhakikisha tunatoa huduma bora za uwakala wa bima na kutumia utaalam wetu katika kujadiliana na wataalam wa masoko katika  kutafuta vifurushi kwa ajili ya wateja wetu.

Thamani Yetu

Utamaduni wa kuaminiana, kuwajibika na uwazi ndio thamani yetu ilipo.

Huduma zetu

Huduma za Bima za vyombo vya moto:

  • Bima kubwa (Comprehesive)
  • Bima ndogo (third party) inayojumuisha changamoto za moto na wizi.
  • Bima ndogo (third party) ya kawaida

Fanya kazi nasi leo

Kwa huduma bora ya Bima za vyombo vya moto, usisite kuwasiliana nasi kupitia njia hizi:

P.O . BOX 1964,
Dar Es Salaam, Tanzania.

Simu/WhatsApp: +255 719 078 498

email: broker@sumajkt.go.tz

au fika ofisini kwetu JKT Mgulani jijini Dar es salaam.