Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri SUMAJKT aridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba 5000 Msomera

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri SUMAJKT aridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba 5000 Msomera

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri SUMAJKT, Meja Jenerali (mstaafu) Mohamed Farah aridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba 5000 katika kijiji cha Msomera, wilayani Handeni. Ameyasema hayo wakati alipoongoza wajumbe wa Bodi hio katika ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa nyumba za makazi, unaojengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMAJKT, ikiwa ni operesheni chini ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Kufahamu undani wa taarifa hio, tafadhali tazama video hii hapa chini;

JENERALI MKUNDA AZINDUA MITAMBO YA MAJI SUMAJKT BOTTLING CO. LTD, AFURAHISHWA NA JITIHADA ZA SHIRIKA

JENERALI MKUNDA AZINDUA MITAMBO YA MAJI SUMAJKT BOTTLING CO. LTD, AFURAHISHWA NA JITIHADA ZA SHIRIKA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini Jenerali Jacob John Mkunda leo tarehe 16 Oktoba 2023 amezindua mitambo ya kuzalisha Maji ya kunywa ya Uhuru Peak katika kiwanda cha SUMAJKT Bottling Co. Limited kilichopo Mgulani JKT Jijini Dar es salaam. Mitambo hiyo yenye thamani ya Tsh Bilioni Moja na milioni 800 inaanza kutumika rasmi kuanzia sasa ili kuongeza ufanisi wa kiwanda ikiwa ni Wingi wa Uzalishaji pamoja na kukidhi hitajio la huduma ya maji nchini. Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Majeshi Jenerali John Mkunda ametoa shukurani kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika…

SUMAJKT yatembelewa na Ugeni kutoka Comoros

SUMAJKT yatembelewa na Ugeni kutoka Comoros

Ugeni kutoka Kisiwa cha Comoro, tarehe 06 Septemba 23 umetembelea Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMAJKT) lililopo Mlalakua jijini Dar es salaam. Ujumbe huo wa watu watano ukiongozwa na Mhe. Gavana Sitti Farouata Mhoudine umefika Makao Makuu ya SUMAJKT kwa ziara ya kikazi na umepokelewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Afisa Mtendaji Mkuu SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele. Mhe. Gavana Sitti Farouata katika ziara hiyo amepata fursa ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUMAJKT kupitia Taarifa fupi iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Utafiti wa SUMAJKT. Luteni Kanali George Wang’ombe.Taarifa hiyo…